Ofisi
za Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki kituo cha televisheni cha
Star na cha redio cha Radio Free Africa (RFA) zimefungwa na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) kwa deni la Sh4.5 bilioni.
Ofisi
hizo zimefungwa leo Alhamisi (Julai 13) na wakala wa TRA, Kampuni ya
Sukah Auction Mart and Court Brokers ya jijini Mwanza.
Meneja
utumishi na utawala wa Sahara Media Group, Raphael Shilatu amesema ni
kweli wana malimbikizo ya madeni yanayotokana na kuhama kutoka mfumo wa
analogia kwenda digitali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni