
Mwanamke aliyejeruhiwa kwa risasi usiku wa kuamkia juzi katika kijiji
cha Ruaruke, wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani, Tabia Mbonde anaendelea na
matibabu katika Hospitali ya Mchukwi, kinyume na taarifa zilizoenea
kwamba amefariki.
Awali iliarifiwa kuwa watu wasiojulikana walimuua kwa kumpiga risasi,
mkazi wa Kijiji cha Ruaruke, wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani, Ramadhani
Mzurui, usiku wa kuamkia juzi na kumjeruhi mguuni kwa risasi mke wa
marehemu ambaye alikimbizwa hospitali kwa matibabu.
Mtandao huu ulifunga safari mpaka hospitalini hapo na kufanikiwa kumpata
majeruhi huyo ambaye alishuhudia mumewe akiuawa kwa risasi na yeye
kukimbilia msituni baada ya kupigwa risasi tano mguuni.
Baada ya tukio hilo, mama huyo anadai alianguka msituni ambako alikuja
kuchukuliwa na Wasamaria wema na kupelekwa hospitali. Mama huyo
amefunguka mengi kuhusu mauaji hayo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni