
Katibu
Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji, Mbunge wa Jimbo la Ndanda,
Cecil Mwambe ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kusini pamoja
na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma, Zubeda Sakuru wanashikiliwa na
Jeshi la Polisi wilayani Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho, viongozi hao walipelekwa
jana kituoni kuhojiwa ambapo Katibu Mkuu Dkt. Mashinji alitakiwa kueleza
kwanini yuko Mbamba Bay na aeleze amekwenda kufanya nini.
Polisi
walimkamata Katibu Mkuu Dkt. Mashinji, Mbunge Mwambe na Mbunge Zubeda
baada ya kuvamia kikao cha ndani kilichokuwa kikiendelea mjini hapo
ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu Dkt. Mashinji kukagua shughuli
za chama katika majimbo ya kanda hiyo iliyoanza jana, ilieleza taarifa
hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni