
Wengi wetu wakisikia neno Simba huwa kuna picha flani kwa
haraka inajengeka akilini mwao. Kwa wakazi wa Afrika mashariki, hasa wapenzi wa
Mpira wa miguu , hasa hasa Tanzania picha ya kwanza ni ya simba yule wa
msimbazi (Timu kubwa ya mpira
ijulikanayo kwa jina hilo). Lakini kwa wengine jina au neno hilo lina maanisha
mnyama mkubwa na hatari . kwa leo mnyama huyo ndie nnayemleta kwako katika
uchambuzi yakinifu.
Simba
ambaye jina lake la kisayansi ni Panthera leo ni mnyama
mkubwa kwanye kundi la wanyama wala nyama wa familia
ya felidae katika ngeli ya mamalia.
Kwa maana hii ni kwamba simba ni mnyama ambaye hufanana na
paka mkubwa.
Zamani katika
bara ya Asia Simba walipatikana kati ya Uturuki
na Bangladesh
lakini inakadiliwa kuwa ni simba 300 pekee waliobaki katika hifadhi huko Gujarat
nchini Uhindi. Kulikuwa
na aina nyingine za simba waliopatikana Ulaya na pia Afrika ya kaskazini lakini
zote zimekwisha kwa sababu nyingi ikiwemo kuwindwa vikali.
Kwa kwawida
chakula
chao ni nyama
ambayo inapatikana kwa kuwinda wanyama wengine hasa wala majani. Tofauti na
paka wengine, simba huishi katika makundi na huwinda katika vikundi vyenye simba
10-20. Kila kundi lina eneo lake na hulitetea
eneo hilo dhidi ya simba wengine.
Simba dume huweza kufikia urefu wa mwili wake wote sentimita
170 hadi 250, kimo cha mabegani ni sentimita 120. Ambapo anaweza kufikisha uzito wa kilogramu
225.

Simba jike huwa na umbo dogo ukilinganisha na
lile la dume akiwa na urefu wa sentimita140 hadi 175, kimo cha mabegani cha
sentimita 100 na uzito wa kg 150.
Dume na
jike hutofautishwa kirahisi kutokana na manyoya marefu ya shingoni
mwa simba dume ilhali jike hana. Miongoni mwa jamii ya paka, simba ndio pekee
wenye tofauti ya moja kwa moja ya muonekano baina ya dume na jike. Simba dume
na simba jike huonekana tofauti kabisa. Pia wana kazi tofauti wanazofanya
katika makundi yao. Kwa mfano, simba jike, wawindaji, hawana nywele kichwani kama ilivyo kwa simba
dume. Huonekana kumzuia simba jike wakati anapokuwa ananyatia mnyama na
kusababisha joto zaidi wakati wa kukimbiza windo lake.
Rangi ya nywele za simba dume ni tofauti, kuanzia ile kama ya dhahabu
mpaka nyeusi, na mara nyingi huwa nyeusi zaidi
kadiri simba anavyozeeka.
Uzazi wa
simba huanza pale Jike anapofikia umri wa miaka 2-3. Baada ya kuwa mjamzito kwa miezi 3 na nusu anazaa simba wadogo 2 hadi 3. Wakati mwingine idadi hii inaweza kuongezeka hadi kufikia 6 lakini wanaozidi 3 kwa kawaida
wanakufa mapema. Wakati wa kujamiana, dume hutoa shahawa
mara 20 mpaka 40 kwa siku kadhaa.
Wengi wa
simba jike huanza kuzaa wakiwa na miaka minne. Simba hawajamiani katika kipindi
maalumu cha mwaka, Kama ilivyo kwa paka wengine, uume wa simba una kama
miiba iliyogeukia nyuma. Wakati wa kuutoa, miiba hiyo hukwangua kuta za uke na kusababisha
kuachiwa kwa yai.
Akiwa kwenye joto, simba jike huweza kujamiana na zaidi ya dume mmojana
mjamiiano huu unaweza kuchukua siku kadhaa, wenza hao hujamiana mara ishirini
mpaka arobaini
kwa siku na mara nyingi hata huahirisha kula. Simba huzaliana vizuri kwenye
hifadhi.
Simba
jike hubeba ujauzito
kwa siku 110, mara nyingi mbali na lilipo kundi lake. Mara nyingi huwinda peke
yake wakati watoto bado hawajiwezi, watoto hawa huzaliwa wakiwa hawaoni, mpaka
baada ya wiki moja.
Huwa na
uzito wa kg 1.2 mpaka 2.1 wakati wa kuzaliwa na huweza kuanza kutambaa baada ya
siku moja mpaka mbili na kuweza kutembea nje baada ya majuma matatu. Simba jike
huyo huwahamisha watoto wake mara kadhaa kwa mwezi, kwa kuwabeba mmojammoja kwa
shingo zao, ili kuzuia harufu kujijenga kwenye malazi yao na
hivyo kuvuta wanyama wengine wala nyama ambao pengine wangeweza kuwadhuru
watoto.
Karibu
miaka 10,000 iliyopita, simba walikuwa ndio wanyama wa nchi kavu waliotawanyika
zaidi baada ya binadamu.
Walipatikana hasa Afrika, Mashariki mwa Ulaya mpaka Asia, na Amerika
kuanzia Yukon
mpaka Peru.
Simba
huishi kwa wastani wa miaka 10-14 msituni, huku katika hifadhi huweza hata
kufika zaidi ya miaka 20. Msituni, simba dume ni mara chache kuishi zaidi ya
miaka kumi,
sababu ya majeraha wanayoyapata kwa kupigana na dume wengine mara kwa mara. Hupatikana
sana katika savanna
na nyika, ingawa pia huweza kukaa kwenye nyika
na vichaka.
Simba,
tofauti na paka wengine, huweza kuchangamana kwa urahisi. Kundi la simba
hujumuisha simba jike ndugu kadhaa na watoto na idadi ndogo ya simba dume
wakubwa. Kundi la simba jike huwinda pamoja, hasa huwinda wanyama wenye kwato. Simba huwinda wenyewe japo mara
kadhaa huonekana wakila mizoga. Wakati simba kwa kawaida hawawindwi
na binadamu, wachache wam
eripotiwa kumla na hivyo kumwinda.
Simba ni
miongoni mwa spishi iliyo hatarini kutoweka, na kuonekana kupungua kutoka kwa
asilimia 30 mpaka hivi sasa kwa asilimia 50. Japo sababu kubwa ya kupungua huku
haijulikani, kupungua kwa uoto na mwingiliano na binadamu imekuwa
kama sababu kubwa za kupungua kwao. Tangu enzi za ngome
ya Roma, simba wamekuwa spishi kuu inayotafutwa kwa ajili ya maonesho kwenye
[zoo] duniani, hasa tangu mwishoni mwa karne ya 18.
Simba wapatikanao asia Asia ndio walio
athilika sana na suala hilo.
Kati ya
wanyama wote wa jamii ya paka, simba ndiyo mrefu (mabegani), na ndio wa pili
kwa uzito baada ya tiger. Kwa miguu yake yenye nguvu, taya imara, na meno yake chonge yenye
urefu wa sm 8, simba anaweza akamwangusha na kumuua myama mkubwa. Fuvu la
kichwa la simba linafanana sana na lile la tiger, hivyo tofauti ya taya zao za
chini ndio pekee hutumika kuwatofautisha.
Mifupa ya
simba wa kale zaidi ilipatikana Laetoli,
Tanzania,
na ni la karibu miaka milioni 3.5 iliyopita. Wanasayansi kadhaa waliita
mabaki haya Panthera leo. Rekodi hizi
hazijathibitishwa sana na kinachoweza kusemwa ni kuwa zinakaribiana na zile za
Panthera. Panthera aliyethibitishwa ni yule wa miaka milioni 2 iliyopita.
Aina nyingine
zilizokaribia Panthera ni: tiger, jaguar na chui. Tafiti za maumbo na chembe za uhai zinaonesha
kuwa tiger ndio alikuwa aina ya kwanza kutokea miongoni mwa aina myingine hizi.
Miaka milioni 1.9 iliyopita jaguar alijitokeza, ambaye kutoka kwake ndiyo
tunapata chui na simba. Simba na chui walitengana kamili miaka milioni 1.25
iliyopita.
Panthera
leo alijitokeza Afrika miaka milioni 1.8 iliyopita, kabla ya kusambaa Afrika
kwenye ukanda wa Holarctic. Kwa mara ya kwanza ilionekana Ulaya miaka 700,000
na huko Amerika miaka 300,000 iliyopita.
Rangi ya simba hubadilika
kutoka rangi ya manjano mpaka njano, nyekundu
na kahawia ya kukoza. Sehemu za chini huwa na
rangi angavu na kishungi cha mkia wake ni cheusi. Watoto wa simba
huzaliwa na madoa meusi mwilini mwao, kama vile wale wa chui. Japokuwa madoa
haya hupotea taratibu wakati wakikua, baadhi ya madoa haya huendelea kuonekana
miguuni na sehemu za chini za mwili, hasa kwa simba jike..
Simba
hutumia muda wao mwingi wa siku kupumzika kwa takriban saa 20 kwa siku.
Japokuwa wanaweza kuamka muda wowote, lakini usiku mpaka mapambazuko hutumiwa kwa
kuwinda. Hutumia wastani wa saa mbili kwa siku kutembea na dakika
50 kula. simba wana meno makali sana, lakini mawindo yake daima huuwawa kwa
kunyogwa.
Simba ni
wanyama wenye nguvu ambao mara zote huwinda kwa makundi na kumkazania windo
walilochagua. Na huweza kufikia mwendokasi wa kilomita 81
kwa saa, wanaweza kufanya hivyo kwa mwendo mfupi tu na inawapasa kuwa karibu na
mawindo kabla ya kuanza shambulio. Hufanya uwindaji sana nyakati za usiku.
Humnyatia adui mpaka pale wamekaribia kwa walau mita 30 au pungufu. Kisha
kukaribia huchagua mnyama aliye karibu. Shambulio huwa fupi na la nguvu;
hujaribu kumkamata kwa kumkurupusha kwa kasi na kisha kumrukia.

Mnyama huyo
daima huuawa kwa kunyongwa. Mara kadhaa pia huweza kuuawa kwa kuzibwa mdomo na pua zake kwa taya za
simba. Wanyama wadogo huuawa tu kwa kupigwa ngwala
kwa mguu wa simba.
Kitoweo cha simba hujumuisha wanyama wengi
wakubwa, hasa nyati, swala, pundamilia,
na aina kadhaa za tandala huko India. Spishi nyingine huwindwa kutokana na
upatikanaji wao.
Simba
wakiwa wanawinda katika kundi kubwa wana uwezo hata wa kuangusha wanyama
wakubwa lakini mara nyingi huwa hawashambulii wanyama wakubwa sana kama vile twiga kwa kuhofia
kujeruhiwa pia.
Simba
pia wana uwezo wa kushambulia wanyama wanaofugwa na binadamu; kwa mfano huko
India ng’ombe
wengi huwa chakula cha simba. Simba pia wanaweza kula wanyama wenzao wanaokula
nyama kama vile chui, duma,
fisi na mbwa mwitu. Pia wakati
mwingine hula mizoga ya wanyama wengine waliouawa kwa majanga au na wanyama
wengine, na huangalia sana mahali wapozungukazunguka tai, wakijua fika mahali
walipo patakuwa na mizoga.
Simba
anaweza kula mpaka kilo 30 kwa mlo mmoja; na kama hawezi kula windo lake
lote, hupumzika kwa saa kadhaa na kisha kuendelea tena. Wakati wa mchana
na joto kali, kundi la simba hukaa kivulini na dume mmoja au wawili kubakia
kama walinzi. Simba jike anahitaji walau kg 5 za nyama kwa siku wakati dume ni
kg 7.
Kwa
sababu simba huwinda kwenye sehemu wazi, ambapo wanaonekana kwa urahisi na adui
zake, uwindaji wa ushirikiano ndio husaidia na
kufanikiwa, hasa kwa wanyama wakubwa. Ushirikiano huu husaidia pia kulinda
mawindo yao kwa urahisi dhidi ya wanyama wengine, kama vile fisi, ambao mara
moja hujua mzoga ulipo kwa kuangalia mahali ambapo tai wanaruka. simba dume
waliopo kwenye kundi hawashiriki kwenye uwindaji mpaka tu pale wanapohitaji
kuwinda wanyama wakubwa kama vile twiga au nyati. Wakati wa kuwinda kila simba
jike ana nafasi ya kuwinda na kumpata mnyama, aidha kwa kunyatia na kisha
kushambulia au kusogea umbali kidogo karibu na katikati mwa kundi na kumkamata mnyama
huyo amwindaye kutoka kwa simba wengine.
Simba
wadogo huanza huonesha tabia ya kunyatia wanyama wakiwa na miezi mitatu tu,
ingawa hawashiriki kwenye uwindaji mpaka wawe na umri wa mwaka mmoja. Huanza
rasmi kuwinda wakiwa na umri wa miaka miwili.
Huyo ndio simba
JibuFuta