Jumatatu, 19 Juni 2017

Filamu ya Tupac ‘All Eyes On Me’ yaingiza $27m



Japo mwanzoni filamu hiyo ilionekana kupondwa na mastaa kadhaa akiwemo Jada Pinkett Smith, lakini imeshika nafasi ya tatu kwa kuingiza dola milioni 27 katika wiki yake ya kwanza.
Filamu hiyo imeongozwa na Benny Boom na Demetrius Shipp ameigiza kama Tupac huku Danai Gurira akiigiza nafasi ya Afeni Shakur ambaye ni mama mzazi wa rapper huyo ambaye alifariki mwezi Mei, mwaka huu kwa tatizo la mshtuko wa moyo.
Filamu hiyo iliachiwa siku ya birthday ya Tupac, Ijumaa ya Juni 16 ambao rapper huyo angekuwa na miaka 46.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni