Producer huyo ambaye ametengeneza ngoma kama ‘Tumeoana’ ya kundi hilo, amedai analipwa kila anapofanya kazi na kundi hilo ambapo pia amedai hana tatizo na wasanii wanaounda kundi hilo.
“Hizo ni stori zimetengenezwa, kwanza mie ndio nimetoa jina la The Amaizing, tena nilipigiwa simu na wenyewe wakaniambia kuwa wanaunda kundi linaitwa Amaizing, mie ndio nikasema mbona Amaizing kama linahang nikatoa wekeni The Amaizing, hizo stori zimetengenezwa,” amesema Dupy
Pia producer huyo mwenye maskani yake Mbagala amethibitisha kuwa yeye na Izzo ni good friends na ni kama brother na sio hivyo tu yaani bado wapo pamoja na wanatengeneza mdundo mwingine ambao utakuja kuchukua nafasi ya ‘Tumeoana”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni